Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Katibu wa Tume Bw. Nyakimura Muhoji (kulia) akifafanua kuhusu jukumu la Urekebu la Tume katika kushughulikia rufaa na malalamiko ya watumishi wa Umma. Kushoto ni Bw. Peleleja Masesa,Katibu Msaidizi wa Tume, tarehe 30/5/2017 Kamati ya Maadili ya Tume ya Utumishi wa Umma ikibadilishana uzoefu wa utendaji kazi na Kamati ya Maadili ya Mamlaka ya Mawasiliano ya Malawi na baadhi ya Maafisa wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Malawi, tarehe 28/7/2017 Afisa Msimamizi wa UNDP - Tanzania Bw. David Omozuafoh (aliyekaa wa pili kutoka kushoto) na Bi Natalie Rolloda (wa kwanza kushoto) katika picha ya pamoja na M/kiti wa Tume (Jaji Mstaafu) Dk. Steven Bwana (aliyekaa katikati) pamoja na menejimenti ya Tume M/kiti wa Tume ya Utumishi wa Umma (Jaji Mstaafu) Dk. Steven Bwana (mbele katikati) akizungumza katika kikao cha pamoja na Maafisa kutoka UNDP - Tanzania Bw. David Omozuafoh na Bi Natalie Rolloda (kulia) walipoitembelea Tume, Septemba 5, 2017 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo kwa watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es Salaam. Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji akizungumza na Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu katika Mkoa wa Lindi, Tume ilipofanya ziara katika mkoa huo kwa lengo la kuwajengea uwezo katika masuala ya usimamizi wa rasilimali watu. Kamishna wa Tume ya utumishi wa Umma Bi. Salome Mollel (wa nne kutoka kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (katikati) , Tume ilipofanya ziara ya kikazi katika mkoa huo Novemba 02 hadi 03, 2017. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (Mb) akimkabidhi Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji Mwongozo wa Klabu za Maadili za Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo katika uzinduzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu. Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji akitoa neno la shukrani kwa wadau walioshiriki mdahalo kuhusu Maadili na Haki za Binadamu uliofanyika Mkoani Dodoma Novemba 27, 2017 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Emmanuel Kuboja akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Tume ya Utumishi wa Umma mara baada ya kufungua Wiki ya Huduma kwa wadau katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere, Dodoma. Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora , Kapt. (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo kwa watumishi wa Tume ya utumishi wa Umma alipotembea banda la Tume Mkoani Dodoma Disemba 07, 2017 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika banda la Tume ya Utumishi wa Umma akipokea maelezo ya kiutendaji ya ofisi hiyo kutoka kwa Katibu wa Tume Bw. Nyakimura Muhoji katika viwanja vya Mwl. Nyerere Dodoma. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipewa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma Disemba 10, 2017. Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bibi Roselyne Mboya (wa kwanza kulia) na msaidizi wake Bibi Selina Maongezi (katikati) wakitoa elimu kwa umma kupitia kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na kituo chaAzam Televisheni, tarehe 19/6/2018

Karibu Tume ya Utumishi wa Umma

 

Tume ya Utumishi wa Umma imeundwa chini ya Kifungu Na. 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298. Tume ilianza kufanya kazi rasmi tarehe 7/1/2004 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua viongozi ( Mwenyekiti, Makamishna na Katibu wa Tume) kusimamia utendaji wake.

Kazi kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kusimamia uendeshaji wa shughuli za Rasilimali watu katika Taasisi za Umma na kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.

Tume ya Utumishi wa Umma inaendelea kushirikiana na wadau wake wote ili kuhakikisha kuwa U...

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.